Mwezi Aprili 22 Dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Dunia, ambayo huadhimishwa kila mwaka. Siku hii imekuwa ikiadhimishwa na Umoja wa Mataifa kama siku ya kimataifa ya Dunia tangu mwaka 1970.
Ni nini unachokifahamu zaidi kuhusu sayari hii ya dunia?
Andiko hili fupi kupitia blogi hii inakwenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo sayari yetu inayo kama sifa pekee ukiachana na sayari nyinginezo;
1.Dunia sio duara kamili
Kwa kawaida dunia huwa inadhaniwa kuwa ni duara kamili, lakini uhalisi ni kwamba duniani ni duaradufu. Dunia huwa inamesawazishwa kuelekea kwenye maeneo yan cha na kuvimba tena kuelekea maeneo ya ikweta.
Athari hizi husababishwa na sumaku ya dunia na kuzunguka katika mhimili wake. Hivyo basi, mzunguko wa dunia katika ikweta ni una urefu wa karibu kilomita 43 zaidi kuliko mzunguko baina ya ncha za dunia.
2. Asilimia takriban 70 ya dunia imefunikwa na maji

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maji katika dunia yako katika hali ya kimiminika, magumu na gesi.
Karibu theluthi tatu ya uso wa dunia imefunikwa na barafu, maziwa, mabwawa, mito,vijito na bahari.
Karibu 97 asilimia ya maji haya ni maji ya bahari ya chumvi.
2. Anga huanzia katika umbali wa karibu kimomita 100 juu ya usawa wa dunia
Mpaka baina ya hali ya hewa na anga za juu ni kilomita 100 juu ya usawa wa bahari.
Msingi wa dunia umetengenezwa na chuma
Dunia ni sayari ya tano kwa ukubwa katika mfumo wa jua. Na inaaminiwa kuwa ina ukubwa wa eneo wa karibu kilomita 1,200 umeundwa na asilimia 85 ya chuma na asilimia 10 ni nikeli.
4. Dunia ndio sayari pekee yenye maisha
Dunia ndiyo sayari pekee inayofahamika kuwa na viumbe vinavyoishi.
Dunia iliundwa takriban miaka bilioni 4.5 , iliyopita, na historia yake ya kijiografia na setilaiti vimeruhusu maisha kuwepo hapa kwa mamilioni ya miaka
Takriban spishi milioni 1.2 za Wanyama zilirekodiwa kuidhi duniani.
6. Sumaku ya dunia sio sawa kila mahali

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kwasababu sayari Dunia sio duara kamilifu, sumaku/mvuto wa dunia hauko sawa katika maeneo tofauti.
Kwa mfano, kadri unavyotoka katika maeneo ya ikweta kuelekea kwenye maeneo yan cha za dunia, sumaku ya dunia huimarika . Lakini mtu hawezi kuhisi utofauti huu mdogo.
7. Dunia ni sayari yenye utofauti
Utofauti wa kijiografia wa kanda na hali za hewa inamaanisha kuwa kila kanda ina tabia zake tofauti na nyingine.
Kuna sehemu mbali mbali ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa maeneo ya joto zaidi dunaini. Viwango vya juu zaidi vya joto kuwahi kurekodiwa ni vile vilivyotokea katika Death Valley nchini Marekani , ambako mwezi Julai 10, 1913, kipimajoto kilionyesha viwango vay joto kufikia nyuzi joto 56.7.
Kiwango cha chini kabisa cha joto duniani kilirekodiwa Julai , 31, 1983 katika kituo cha Vostok station kilichopo Antarctica: nyuzi joto – 89.2
8. Eneo lenye makazi zaidi katika Dunia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
The Great Barrier Reef kwenye mwambao wa Australia ni eneo linalokaliwa na viumbe hai wengi zaidi linaloweza kutazamwa katika sayari Dunia.
Ukubwa wa eneo hili ni zaidi ya kilomita 2000 na maelfu ya viumbe wa baharini huishi hapa
Katika mwaka 1981, mimea ya coral reef ilijumuishwa katika Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.
9. Dunia ndio sayari pekee katika mfumo wa jua yenye matabaka ya miamba migumu.
Kusogea kwa matabaka haya kunaonyesha kuwa uso wa Dunia unabadilika.
Matabaka haya ya miamba pia yanahusika katika kuundwa kwa miamba mchakato unaosababisha volcano.
Kusogea kwa miamba hii huhakikisha kuwepo kwa mzunguko wa gesi ya hewa chafu kama vile carbon dioxide kwa kuendelea kubadili upya sakafu ya bahari, na wakati huo huo hufanya jukumu muhimu la akudhibiti viwango vya joto vya Dunia.
10. Dunia ina ngao ya kinga

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Eneo la sumaku la Dunia huwa kama ngao dhidi ya kupiga kwa mara kwa mara kwa jua na chembechembe zenye joto la juu zaidi.
Eneo hili huanzia kwenye mhimili wa ndai wa dunia hadi kwenye mpaka wake ambako hugongana na upepo wa jua.
CC; BBC Swahili