Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali imejiandaa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini ikiwa ni pamoja na kuwapandisha madaraja na vyeo wafanyakazi nchini
Rais Samia ametioa kauli hiyo mkoani Morogoro katika maadhimisho ya Mei Mosi ambapo amesema serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi
“Hili la mishahara kwa mwaka huu mbali na upandishaji wa posho ambao nimeusema tumejiandaa pia kupandisha madaraja, vyeo vitaendelea kupandishwa, yale madaraja mserereko ambao hawakupata mwaka uliopita mwaka huu yapo” amesema Rais Samia
Kuhusu Nyongeza ya mishahara Rais Samia amesema kuwa serikali imerejesha nyingeza za mishahara za kila mwaka ambazo zilikuwa zimesitishwa kwa muda
“Kuna nyongeza za mishahara za mwaka ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa nikaona mwaka huu tuzirudishe, kwahiyo wafanyakazi wote mwaka huu kuna nyongheza za mishahara za kila mwaka, tunaanza mwaka huu na tutakwenda kila mwaka kama ilivyokuwa zamani”
Aidha Rais Samia amesema kutangaza ni kiasi gani kitaongezwa katika misharara kitaadhiri bei ya vitu mbalimbali hivyo kuwataka wafanyakazi kuwa watulivyo kwani wanachotamani kusikia hawatakisikia ila kitafanyiwa kazi
“Ndugu zangu wafanyakazi kile wtu walichozoea tukiseme hapa ili wapandishe bei madukani mara hii hakuna tunakwenda kufanya mambo polepole, wasione tumeongezeana kitu gani ili mwenendo wetu wa bei uwe salama”