Manchester United ilituma wasaka vipaji kumtazama mshambuliaji wa Roma Tammy Abraham, 25, mwishoni mwa wiki iliyopita huku klabu hiyo ikifikiria mbadala wa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29. (Mirror).
Hata hivyo, Aston Villa wana uhakika wanaweza kumsajili mchezaji wa kimataifa wa England Abraham kutoka Roma – licha ya vilabu kadhaa vikubwa Ulaya kumuwinda nyota huyo. (90Min)