Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua kampeni inayojulikana kwa jina la “TUWAJIBIKE” inayolenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wauzaji wa bidhaa na wananunuzi kutoa na kudai risiti halali za EFD wauzapo na wanunuapo bidhaa zao.
“TRA Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD bila ya kushurutishwa na wanunuzi kudai risiti halali za EFD kwa kila manunuzi watakayoyafanya ili kuepuka usumbufu usio wa lazima, wakati huo huo kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi wa nchi nzima” Richard Kayombo Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Mlipa Kodi TRA
Kampeni hio inafanywa ili kusaidia kukusanya mapato ya kutosha serikalini ili kuweza kufanikisha zaidi ktika masuala ya kiutendaji na kukamilisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini.