Mtangazaji @zamaradimketema amezindua chaneli yake ya Zamaradi TV ambayo itakuwa ikipatikana kwenye king’amuzi cha @azamtvtzchaneli namba 413.
Zamaradi amesema, ameingia kwenye biashara hiyo ya ‘mainstream’ akiwa amejipanga tayari na kuahidi itakuwa ni chaneli ambayo italeta mapindizi makubwa kwenye upande wa Entertainment ikiwa na vipindi tofauti tofauti.
Akizungumza wakati wa uzinduzi akiwa amesindikizwa na mume wake Shaban, Zamaradi amewaomba Watanzania wampokee rasmi kwani amejipanga kuleta utofauti mkubwa kwenye tasnia hiyo.