Kwa miongo kadhaa, kumekuwepo na pengo kati ya wanawake na wanaume kwenye masomo yanayohusiana na Sayansi, Hisabati, Uhandisi, na Teknolojia (STEM).
Ripoti ya hivi karibuni ya GSMA zinaonyesha asilimia 86 ya wanaume nchini wanamiliki simu za mkononi ikilinganishwa na asilimia 77 ya wanawake.
Pia inaonyesha asilimia 17 ya wanawake wanapata huduma ya intaneti, na kwa wanaume ni asilimia 35. Utofauti huu wa ufikiwaji na mtandao wa intaneti unaonyesha changamoto kubwa kwa wanawake kwenye kupunguza pengo la ufikiwaji wa habari na mafunzo mtandaoni pamoja na maarifa ya kisasa ya kidigitali yatakayowawezesha kuwa washindani na kuendena na soko la sasa ambalo ni la kiuchumi wa kidigitali.
Suala hili lisipozungumziwa litabakia kuwa ndoto itakayo athiri uwakilishwaji zaidi wa wanawake kwa miaka ijayo katika masuala ya usimamizi na uongozi katika sekta mbalimbali.
Pengine inaweza kuwa ni hofu ya ripoti ya mwaka 2022 ya UNESCO inayoangazia jinsia, inayoonyesha idadi ya wanawake waliojiunga na masomo yanayohusiana na sayansi kati ya wanaume 100, imeongezeka kutoka 31 mwaka 2000 na kufikia 84 mwaka 2020 Tanzania, ikionyesha muelekeo chanya kuelekea kupunguza pengo lililopo.
Kwa wastani wa idadi ya usaili wa masomo ya elimu ya juu na chuo kikuu nchini kote ikiwa ni zaidi ya wanafunzi 524,000 kwa mwaka 2022, kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU), ni asilimia 3.4 pekee ya idadi hiyo inajumuisha wanawake katika masomo yanayohusu sayansi na takribani mara mbili ya wanaume kwenye masomo hayo.
Lakini hii sio changamoto kwa Tanzania au Afrika pekee kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2017 inayojulikana kama ‘Cracking the Code: Girls’ and Women’s Education in STEM’ ya UNESCO, inaonyesha asilimia ya wanawake kwenye elimu ya juu wanaojifunza masomo ya sayansi ni asilimia 35 duniani.
Mwaka 2018, Vodacom Tanzania ilianzisha programu ya ‘Code Like a Girl’ ili kusaidia kuhamasisha wanafunzi wa kike kujifunza masomo ya sayansi (STEM) na kujua taaluma zinazohusiana nazo.
Programu hiyo imeeendelea kuendeshwa kwa miaka mitano na imewawezesha wanafunzi wa kike zaidi ya 1,700 wa kidato cha tano na sita kujifunza maarifa ya kutengeneza tovuti, aplikesheni, kuandaa ripoti za uwasilishaji, pamoja na kutumia vifaa vya Tehama ili kuendana na mahitaji ya soko la sasa la kidigitali. Programu inaendeshwa kwa kushirikiana na Tanzania Data Lab (dLab).
Kwa mujibu wa Vodacom, wakati matumizi ya teknolojia yamepelekea kuongezeka kwa kuzifikia huduma muhimu na kuboresha uzalishaji katika sekta tofauti, bado kuna uhitaji wa kuwawezesha wanawake na wasichana kunufaika kiukamilifu na mapinduzi ya kidigitali, bila ya kuzingatia umri, kabila, kipato, ulemavu, au sababu nyinginezo za kijamii ambazo zinaweza kukwamisha maendeleo yao.
Hii ilibainishwa mwaka 2021 wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, ambayo ilijikita kwenye kuendeleza maarifa ya kidigitali kwa wanafunzi wa kike.
Vodacom inaitumia teknolojia ipasavyo kuinufaisha jamii kwenye mikoa tofauti ya Tanzania, hususani kupitia jitihada zinazolenda kuwawezesha wanawake na wasichana. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imeshirikiana na wataalamu mbalimbali na kuwekeza katika miradi yenye dhamira ya msingi ya kuwawezesha wasichana na wanawake. Mpaka sasa, zaidi ya wasichana 5,000 wamenufaika na programu mbalimbali za kidigitali ambazo zinatolewa na kampuni.
Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya programu ya ‘Code Like a Girl’ Februari mwaka huu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema; “programu ya Code Like a Girl mwezi wa Februari inasherehekea kuwezesha mafunzo kwa wasichana zaidi ya 1,700 kwenye mikoa tofauti ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya malengo yake ya kuhamasisha kupenda masomo ya sayansi na Tehama na kuwezesha maarifa ya kidigitali kwa wasichana wa umri kati ya miaka 14 mpaka 18 kwa siku nne.
Programu ilihusisha watoa mafunzo mashuhuri ambao ni mfano wa kuigwa kwa wasichana, kuwatia moyo kupenda teknolojia na fursa zinazoambatana nazo”.
Programu hii ilianzishwa ikiwa ni sehemu ya Vodacom kuhakikisha ujumuisha kwenye matumizi ya teknolojia na uunganishwaji katika zama ya kidigitali ambayo itakuwa ni vigumu kuwezekana kutokana na pengo la jinisia lililopo sasa, ukizingatia kwamba idadi ya wanawake ni wengi kuliko wanaume nchini Tanzania.
Ripoti pia inaonyesha kuwa wasichana wadogo ni asilimia 25 pekee ya wanafunzi wacmasomo ya uhandishi au teknolojia ya mawasiliano na habari.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha IoL News ya mwaka jana, nchini Afrika Kusini pekee ni asilimia 13 tu ya wahitimu wa masomo ya sayansi ni wanawake.
Serikali ya Tanzania imejikita zaidi kwenye maendeleo ya elimu ya masomo ya sayansi ili kujiandaa na Dira ya Taifa ya mwaka 2050.
Hii itajenda uwezo wa kuhimili na kuendana na teknolojia ambayo itaongeza uzalishaji katika sekta zote za uzalishaji ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hili liliwekwa wazi na Makamu wa Rais wa Dk Phillip Mpango wakati wa uzinduzi rasmi Dira ya Taifa ya 2050.