Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) imeruhusu Mabasi ya Mikoani kuanza safari zake saa tisa usiku ambapo imeagiza Wamiliki wa Mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wafike katika Ofisi zao kuomba leseni.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy amesema ni lazima Madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao.
Ikumbukwe hapo awali Mabasi yalikuwa yanafanya safari zake kwa kuianza mapema ila ilifikia muda baada ya matukio ya Uhalifu na ajali kukuthiri ndipo mamlaka hio ilidhibiti kwa kutoa tamko rasmi kuwa mabasi yasianze safari zake usiku sana na pia yasiendelee safari zake pindi tu ifikapo saa 6 ya usiku na kuendelea.