Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee ameitaka kamati ya ushauri ya kitaaluma na kitaalam ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kuandika maandiko ambayo yatachochea kukuza uchumi wa Mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla.
“Ni aibu Mkoa wa Mara wenye rasilimali nyingi lakini hazioneshi kuwanufaisha wananchi, kuanzia kwenye ziwa, madini, hifadhi kwahiyo niwaombe Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha Kilimo na Teknlojia kujikita kusaidia katika kuinua uchumi wa wana-Mara sasa”Meja Jenerali Suleiman Mzee, Mkuu wa mkoa wa Mara