Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, anaweza kumfuata hasimu wake Mreno Cristiano Ronaldo, 38, huko Saudi Arabia kwa uhamisho wa pauni milioni 320 kwa mwaka katika nchi ya Ghuba baada ya kuthibitisha kuwa anaondoka Paris St-Germain. (Telegraph)
Klabu ya Saudia ya Al-Hilal huenda ikaingia vitani kuwania saini ya Messi dhidi ya klabu ya Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu, inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United na Uingereza David Beckham. (Guardian)
Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24, mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Mfaransa Moussa Diaby, 23, na nyota wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 30, wa Ivory Coast na Muingereza Marc Guehi, 22, ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na kocha wa Arsenal Mikel Arteta kwenye orodha ya wachezaji sita wa kisajiliwa katika dirisha la msimu wa joto. (Mail)
Tottenham wanamtaka kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na Hispania Xabi Alonso, 41, kuwa mrithi wa Antonio Conte baada ya matakwa ya mshahara ya Julian Nagelsmann kuwatoa Spurs katika mbio za kumpata Mjerumani huyo. (Metro)
Mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst ana nia ya kusalia Manchester United lakini Mashetani Wekundu bado hawajaanza mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuhusu kusalia Old Trafford wakati mkopo wake kutoka Burnley utakapoisha. (Telegraph)CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Weghorst
Klabu ya Ligue 1 ya Marseille itajielekeza kumsajili mchezaji wa Crystal Palace ambaye anamaliza kandarasi yake mwishoni mwa msimu, Zaha ikiwa itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. (FootMercato)
Newcastle inaweza kumnasa winga wa zamani wa Leeds Raphinha wa Barcelona na Brazil na kumrejesha Ligi Kuu England kwa uhamisho wa pauni milioni 70 (Sun)
Real Madrid wako kwenye mazungumzo kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, lakini klabu hiyo ya Ujerumani inasema bado haijapokea ofa kutoka kwa wababe hao wa Uhispania. (Sky Germany)
Sheikh Jassim ameachana na mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 31, ikiwa atafaulu kuinunua Manchester United – badala yake analenga kusajili nyota watatu wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, wa Paris St-German, Kingsley Coman wa Bayern Munich, 26, na Eduardo Camavinga, 20 wa Real Madrid (Bild’s Christian Falk)