MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuweka nguvu katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza michezo kwa Ukanda huo.
Amesema hayo leo Alhamisi (Mei 04, 2023) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV Jijini Arusha.
Amesema kuwa mawaziri hao wawekeze kwenye kujenga uwezo wa kitalaamu ili kuzalisha wanamichezo wanaoweza kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Maendeleo ya Michezo na Maendeleo kupitia Michezo
“Tusikubali kushika mkia kila siku na wala tusikubali kurudi nyuma”. Amesema kuwa lengo la kila taifa ni kuona timu yake inashinda makombe ya Kimataifa hasa Kombe la Dunia. “Tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo na ujuzi pamoja na kushirikiana tunaweza kufikia malengo makubwa kwenye sekta ya michezo”