
Dkt Tulia alitoa agizo hilo bungeni Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Abdullah Juma (CCM) katika swali lake la nyongeza kuitaka TBA kukarabati nyumba zake ambazo nyingi zimechakaa hususani za Dodoma.
“Nyumba za TBA hususani hapa Dodoma zimejengwa muda mrefu na nyingi zimechakaa, je, lini zitaboreshwa ili kuwa salama kwa watumiaji?” Alihoji
Kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ajibu swali hilo, Spika alieleza kuwa wakala huo unashindwa kufanya majukumu yake kutokana na madeni iliyonayo. “Ninasema hivyo kwa kuwa wabunge nina barua zenu zinazoonesha mnadaiwa kodi na TBA. Wabunge wengi mnaodaiwa nawaagiza mkalipe msije mkafukuzwa huko ili TBA nayo itimize majukumu yake,” alisema Dkt Tulia.