Klabu ya Yanga bado inatakiwa kuongeza pointi tatu nyingine muhimu ili kuweza tangazwa Bingwa kwa mara nyingine katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Msimu wa 2022/23.
Klabu hio inashikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi kuu ikiwa imefikisha jumla ya Pointi 71.
Kwa upande wa mtani wao wa jadi kupitia “Kariakoo Derby” Simba SC imejikita nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 64, ikifuatiwa na Azam FC nqafasi ya tatu huku Singida Big Stars ikiendelea kusalia katika nafasi ya nne katiaka msimamo huo wa Ligi.