
Akitoa taarifa hiyo leo May 06,2023, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuwa, Polisi Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na sababu zinazotolewa, wameshaanza uchunguzi kwa Watu mbalimbali, Hospitali alikotibiwa Binti huyo ambapo na wanashirikisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Wadau wengine wa haki jinai”
Aidha Jeshi hilo limetoa wito kwa Mtu yeyote mwenye taarifa zilizosahihi na zenye ukweli asisite kuwapa Polisi taarifa hizo ili kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo.
“Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika taarifa kamili ya kilichobainika itatolewa kwa umma kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Nchi”