
Klabu ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la #ASFC kwa kuwafunga Simba SC magoli 2-1 katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Azam FC walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Lusajo Mwaikenda dakika ya 22′ dakika 6 baaadae (Yani dakika ya 28) Simba walisawazisha bao hilo kupitia kwa nyota wao Sadio Kanoute.
Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika timu zote mbili zilikuwa zimefungana goli 1-1. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote zilianza kwa kushambulia kwa zamu na dakika ya 75 Prince Dube alifungia Azam FC bao la pili.
Simba waliendelea kutafuta bao la kusawazisha lakini mambo yakazidi kuwa magumu kwao na kupelekea mfungaji wa goli lao Sadio Kanoute kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87 na kufanya Simba kucheza pungufu mpaka dakika 90 zinakamilika.
Azam FC wametinga Fainali ya Kombe la ASFC kwa mara tatu na wanasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Yanga SC dhidi ya Singida Big Stars.
