Kamati ya nidhamu ya CAF imeitoza klabu ya Yanga faini ya jumla ya dola elfu 35 (takribani milioni 82 za Tanzania) kwa matukio kadhaa kuhusiana na mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ya Nigeria iliyofanyika 30 Aprili mwaka 2023.
Yanga SC imetozwa faini ya dola elfu 10,000 kwa matumizi ya fataki na vitocho kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Pia Yanga imetozwa faini ya dola elfu 25 ($25,000) kutokana na tukio la basi waliokuwa wamepanda Rivers United kuvamiwa na kuibiwa pesa takribani dolla 5,200 na kupuliziwa kemikali inayodaiwa kuwa ni sumu kwenye chumba chao cha kubadilishia mavazi.
Pesa hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 60 huku Yanga ikipewa siku tatu za kukata rufaa baada ya siku ya kutolewa kwa uamuzi huo.