
Ikirejerewa ripoti ya matokeo ya sensa ya Tanzania yaliyotangazwa mwaka 2022 yakionesha kuwa Tanzania ina watu wasiopungua milioni 61 na laki saba, kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA imeonesha kuwa hadi March 2023 idadi ya laini za simu zilizopo kwenye matumizi hapa nchini ni Milioni 58.1
Kwa kuzingatia idadi hiyo Dar es salaam imeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika ‘active simcards) kuliko Mkoa mwingine wowote.
1. DSM – 10,936,342
2. Mwanza 3,958,286
3. Arusha 3,713,004
4. Mbeya 3,591,274
5. Dodoma 3,216,101