Jumla ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa mundombinu 48 yenye thamani ya Sh234.12 bilioni imesainiwa na Wizara ya Kilimo katika mwaka 2022/23.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2023/24, leo Jumatatu Mei 8, 2023, Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema ujenzi huo unafanyika kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Amesema tume hiyo inaendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji nchini ikiwemo mabwawa ya kuvunia maji ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji.

“Hadi kufikia Aprili, 2023 eneo linalomwagiliwa ni hekta 727,280.6 sawa na asilimia 60.6 ya lengo la hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025,”amesema.
Amesema tume imeendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji iliyopangwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo hadi kufikia Aprili, 2023 jumla ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miradi 48 yenye thamani ya Sh234.12 bilioni imesainiwa.
Amesema kukamilika kwa kazi zilizopangwa katika mwaka 2022/2023 kutaongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 95,005 na hivyo kufanya eneo linalomwagiliwa kuwa hekta 822,285.6 sawa na asilimia 68.5 ya lengo la kufikia hekta 1.2 milioni za umwagiliaji ifikapo mwaka 2025.