Akizungumza wakati wa kikao kazi Cha tathimini awamu ya kwanza na kuweka mikakati ya awamu ya pili,CPA, Makalla ameelekeza watendaji kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Mitaa kusimamia ufanyaji Usafi.
Aidha CPA, Makalla amesema miongoni mwa mambo yayopaswa kuwekewa mkazo zaidi ni udhibiti wa ufanyaji biashara holela, usafishaji mazingira, upendezeshaji na upandaji miti kwenye bustani.
Kutokana na Mwamko mkubwa wa usafi uliopo, RC Makalla ameelekeza Kila Halmashauri kushirikiana na wadau ambao wapo tayari kupendezesha Jiji huku akielekeza Taasisi za TANROAD, TARURA na DAWASA kufanya kazi kwa ushirikiano.
Pamoja na hayo CPA, Makalla amesema lengo la kampeni hiyo ni kufanya Dar es salaam izidi kushika nafasi za juu kwa usafi Afrika jambo litakalosaidia kudhibiti pia mlipuko wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu na hata kudhibiti maambukizi ya malaria.
Hata hivyo RC Makalla ameendelea kusisitiza Wananchi kufanya usafi Kila ifikapo jumamos ya mwisho wa Mwezi huku akiwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye Maeneo waliyopangwa.