MBUNGE wa Viti Maalum Halima Mdee katika mkutano wa Bunge la leo ametoa maoni yake juu ya mabadiliko ambayo yanatakiwa kuzingatiwa katika Sekta ya Kilimo ili hadi kizazi kijacho kije kuiona tija yake.
Nchini Kenya kwa parachichi wakulima wadogo wadogo ndio wanachangia 85% ya uzalishaji wa parachichi na 15% iliyobaki ni uzalishaji kutoka kwa wakulima wakubwa na kuifanya Kenya kuwa nchi inayoongoza kuuza parachichi nje. Ni vizuri kuwa na wakulima wakubwa lakini tuwasaidie na tusiwasahau wakulima wetu” @halimamdee, mbunge viti maalum
“Waziri wa Kilimo ambaye hana dhamana ya ardhi, ana jukumu la kugawa hekta milioni 1 za ardhi ya nchi hii wakati hatuna taarifa ya hali ya ardhi ikoje”
“kila siku huwa nasema tuangalie kizazi kunachokuja na tusiangalie sasa, Waziri wa Kilimo katika hotuba yake anasema 2050 tutakuwa na Watanzania milioni 139 kutoka milioni 61 hivi sasa, wakati huo huo sensa inaonesha kuwa asilimia 44 ni watoto chini ya miaka 18, sipingi vijana kugaiwa ardhi, napinga concept (wazo) la Wizara ya Kilimo kutafuta wakulima kama ambavyo tunatafuta manesi na walimu”
“Hata hizo block farms (mashamba ya pamoja) bila kuwa na mwekezaji mkubwa, hii program haiwezi kufanikiwa” @halimamdee, mbunge viti maalum
“Wastani wa kusafisha, kusawazisha, kuweka udongo na miundombinu ya umwagiliaji kwa ekari moja ni wastani wa shilingi milioni 16.8, hivi mkulima anaweza kufanya shughuli hizi kwa gharama hiyo ya milioni 16.8?” @halimamdee, mbunge viti maalum
“Tusifanye kilimo cha siasa au kilimo cha kuangalia uchaguzi wa 2025, tufanye kilimo kwa kuangalia kizazi kijacho,na pia Waziri @HusseinBashe tunataka utaumbie kuanzia mwaka ujao wa fedha mafungu yaliyobaki yataingizwa vipi kwa wakulima wadogo”@halimamdee, mbunge viti maalum