Msanii maaufu wa Bongo Fleva Harmonize kupitia ukarasa wa akaunti yake ya Instagram amefunguka kuwa kwa sasa yupo tena kwenye mahusiano mapya na amejidhatiti katika hilo baada ya kutowepo kwa muda mrefu katika mahusiano tangu alipoachana na mpenzi wake wa zamani Kajala Masanja.
Harmonize kwa siku za karibuni amekuwa aki-post matukio yakiashiria yupo na mdada mrembo anayefahamika kama “PHIONA”, awali ameeleza kwa kumsifu mwanamke huyo, halafu akaahidi kuchora tattoo yenye sura ya mrembo huyo kama ya mwisho na kisha akaujuza umma kuwa kwa sasa hayupo “SINGLE AGAIN”
Akiendelea kutikisa chats za Majukwaa mbalimbali ya Kimtandao Duniani kupitia ngoma yake ya Single Again, kwa jinsi anavyounganisha matukio huenda wimbo wake ukasikilizwa zaidi na zaidi kwani hata hivyo umeshawafikia wengi.