Kikosi cha Marumo Gallants kimeshawasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mapema alfajiri kutokea nhini Afrika Kusini kwaajili ya mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF utakaochezwa kesho Jumatano saa 10:00 jioni katika Dimba la Benjanini Mkapa, Manispaa ya Temeke.
Baada ya kuwasili klabu hio imegoma kutumia usafiri ulioandaliwa na wenyeji wao kwa kutumia usafiri mwingine mbadala wake
Mechi hio itawakutanisha miamba hio kutokea Afrika ya Kusini dhidi ya Yanga SC ya hapa nchini ili kuweza kujitengenezea nafasi ya kupata ushindi wa kutinga hatua ya Fainali katika Michuano hio.
Yanga ndio Timu pekee iliyosalia kuiwakilisha nchi katika michuano hio ya CAF Barani Afrika.