Mshauri wa soka wa Paris St-Germain Luis Campos amezungumza na wakala wa Jose Mourinho kuhusu uwezekano wa kocha huyo wa Roma kujiunga na klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu wa joto. (RMC Sport – kwa Kifaransa)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Aidha mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, ambaye kandarasi yake na PSG inamalizika majira ya joto, bado hajafikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 hatarajiwi kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake hadi mwisho wa msimu wa Ufaransa. tarehe 3 Juni. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)