Cristiano Ronaldo amsukuma mfanyakazi wa timu ya pinzani baada ya mfanyakazi huyo kujaribu kupiga picha ‘selfie’ kufuatia sare ya 1-1 kati ya Al-Nassr na Al-Khaleej.
Baada ya mchezo huo kumalizika Ronaldo alikumbwa na maombi kutoka kwa wachezaji wa Al-Khaleej na baadhi ya wafanyakazi klabu hiyo wakitaka jezi yake, alifanikiwa kumpa jezi mmoja ya mchezaji.
Hata hivyo, Ronaldo alionekana akijibu kwa kufoka wakati mmoja wa mfanyikazi wa klabu ya Al-Khaleej alipojaribu kupiga picha naye na kuishia kumsukuma mtu huyo.
Ilikuwa siku ya kufadhaisha kwa Ronaldo, huku matokeo yafifisha matumaini ya Al-Nassr kushinda taji la Saudi Pro League. Mchezo unaofuata Al Nassr watakuwa ugenini kuvaana na RAl-Ta’ee Mei 16 mwaka huu.
Tangu kuhamia kwake Al-Nassr Ronaldo amefunga mabao 12 katika mechi 13 za ligi. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinasema huenda mpinzani wake wa muda mrefu Lionel Messi, akizingatia ofa ya pauni milioni 320 kwa mwaka kutoka kwa Al-Hilal wapinzani wa Al Nassr.
Messi anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain msimu huu wa joto na huenda akajiunga na Al-Hilal na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Sergio Busquets na Jordi Alba.
Imeandikwa na Shabani Rapwi ✍️