Mbunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam Askofu Dkt. Josephat Gwajima ahoji kwa namna ya pekee kutaka kujua Serikali inakwama wapi ili kuweza kutimiza hatima yake ya kuwekeza katika mfumo wa kilimo cha umwagiliaji ili kuweza achana kabisa na dhana ya utegemezi wa misimu ya mvua ambazo kwa sasa imekuwa haitabiliki kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
“Ni kitu gani kinatuzuia kuwekeza kwenye umwagiliaji na hatimaye tukahama kabisa katika kilimo cha kutegemea mvua na kuingia katika kilimo cha umwagiliaji” Askofu Dkt. Josephat Gwajima, mbunge wa jimbo la Kawe
#KoncepttvUpdates