Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu amefanya teuzi mbili za Wenyeviti katika nafasi mbili tofauti za maeneo ya utendaji ili kuweza saidia utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.
Amemteua Prof. Elifas Tozo Busanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa UNESCO ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Prof. Bisanda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa tume hio kwa kipindi cha pili.
Aidha amemteua Mhandisi Abdallah Mohamed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji.
Uteuzi huo wa Wenyeviti umeanza rasmi tarehe 05 Mei, 2023.