Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema kitendo cha Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara kuvua koti na tai akiwa ndani ya Bunge ni utovu wa nidhamu.
Dkt. Tulia ametoa kauli jana Mei 9, 2023 wakati akihitimisha kikao cha Bunge jijini Dodoma baada ya kusoma muongozo wa maswali ambayo baadhi ya wabunge hawakuridhika na majibu yake.
Spika Tulia amesema kitendo hicho kwa mujibu wa kanuni za bunge hakikibaliki ikiwemo vitendo vingine vya kupiga magoti na sarakasi ambavyo tayari alikwisha vikemea.
“Kitendo cha waitara kuvua tai na koti ndani ya bunge ni kulidharau na kushusha hadhi ya bunge hairuhusiwi na isijirudie tena kama una hasira kaanzie nje”
#KocepttvUpdates