Tamthilia hizi zimebeba simulizi za kuvutia ,waigizaji wenye vipaji na viwango vya juu vya utayarishaji na kamera angavu, tukiendeleza dhamira yetu ya kutoa burudani ya hali ya juu kwa watangazaji wetu
“Mchongo” na “Ripoti” zimesanifiwa kwa uangalifu ili kuwapa watazamaji aina mbalimbali za usimulizi wa hadithi zenye kulinda maadili ya kitanzania kutoa elimu kwa jamii na zinazotazamika na familia yote.
Mfululizo huu unaonyesha urithi tajiri wa kitamaduni na talanta ya tasnia ya burudani nchini huku pia ukishughulikia mada za kisasa zinazovutia hadhira pana. Ni imani yetu mchongo na Ripoti zitakuwa MUST WATCH hakuna kukosa wala hatumwi mtoto sokoni.
“Mchongo” Hii ni tamthilia inayohusu msichana wa kazi aliyefungwa kifungo cha maisha jera kwa kosa la kusingiziwa kuua na hivyo kupoteza haki za malezi kwa mtoto wake. Anatoka jera kwa msamaha wa Rais na hivyo kuamua kulipiza kisasi kwa wale wote waliohusika. Azimio Lake linakubwa na vikwazo kutoka kwa mtoto wake mwenyewe ambae anahamini mama yake ni muuaji, pamoja na watu waliomzunguka ambao wanahamini kuwa yeye ni kichaa na anafaa kuishi kwenye hospital ya vichaa. Tamthilia ni mchanganyiko na maisha ya kisasa na maisha ya kawaida ya uswahilini. Tamthilia hii inazalishwa na kampuni ya nexus entertainment na miongoni mwa wasanii mashuhuri walioshiriki katika hii ni pamoja na shamira Ndwangila (Bi star) Suzan Lewis (Natasha) Mayasa Mrisho, Novartis Mayanja, Hidaya Bolli, Majariwa Faki, na wasanii wengine wengi waliopo katika tathinia na wale wanaochipukia.
“Ripoti” Ni tamthiliya inayohusu maisha ya Mfanyabiashara tajiri aliyeoa mwanamke anayejali utajiri na kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii huku akisahau jukumu zima la malezi ya watoto wao hali inayosababisha watoto kujilea na hivyo kuwa mwiba kwa jamii na familia zao. Maisha ya familia hii yanagubikwa na sintofahamu baada ya baba mwenye nyumba “mfanyabiashara tajiri” kupewa taarifa za uongo na madaktari kuwa anaumwa ugojwa wa kansa mpango uliosukwa na mke wake kwa kushilikiana na madaktari ili aweze kurithi Mali zote. Tamthilia hii imeandaliwa na Jerusalem film chini ya muandaaji na msanii mzoefu nchini Jacob Stephen (JB) na miongoni mwa waigizaji mashuhuri katika tamthilia hii ni pamoja na JB mwenyewe, Maria Robert, kessy kambwita, shamsa Ford, Masha Ally, mzee Onyango, na wasanii wengine wengi wanaofanya vizuri katika tasnia ya film Tanzania
“Mchongo” na “Ripoti” zimetayalishwa kwa ustadi, zikishirikisha waigizaji mahili waandishi wenye ujuzi, na watayarishaji wazoefu. Tamthilia hizi zinajumuisha viwango vya juu vya uzalishaji na mbinu za hali ya juu ili kuhakikisha utazamaji wa kuvutia kwa hadhira
“Mchongo” na “Ripoti” zitaonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe (26 na 29 mei 2023 ) na zitarushwa katika chaneli ya sinema zetu pekee.
Tamthilia hizi zinachukua nafasi ya kosa moja itakayokamilika tarehe 20 mei 2023 na zahanati ya kijiji itakayofikia tamati 25 mei 2023