Kocha mkuu wa Yanga SC Nasreddine Nabi amefunguka kuwa licha ya timu yake kupata ushindi wa Goli 2-0 dhidi ya Marumo Gallants katika Mechi ya kwanza hatua ya Nusu Fainali Shirikisho CAF iliyochezwa jana Mei 10 katika dimba la Benjamin Mkapa bado hajafurahishwa na namna kikosi cha klabu hio kilivyocheza kwani amethibitisha kuwa hakijafuata maelekezo aliyoyatoa (Game Plan) kwaajili mya kuukabili mchezo huo.
Aidha ametaka kila mchezaji aweze timiza wajibu wake kwa kuzingatia maelekezo aliyotoa na kujitoa zaidi katika mechi ya marudiano itakayochezwa Mei 17, 2023 huko nchini Afrika Kusini.
“Tumepata Ushindi lakini Sijafurahishwa na namna wachezaji wangu wamecheza, wamecheza tofauti na nilivyowaelekeza wacheze kwa maana hiyo mechi ya marejeano kila mchezaji anapaswa kujitoa na kutimiza wajibu wake uwanjani” Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu Yanga SC.