Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amesema kwamba Viongozi kwa upande wa klabu hio hawana tena hofu ya kuja zungumza mbele ya watu kwakuwa kwa namna timu inavyofanya vyema katika michuano inayoendelea inawaweka vifua mbele na kutoomba watu radhi kila mara wajapo mbele ya Vyombo vya habari.
Ameeleza hayo kufuatia Klabu hio imeshashinda na kuwa na pointi nyingi katika Ligi kuu ya NBC na hapo kesho itaenda kuchuana vikali na klabu ya Dodoma Jiji ikitokea panapo majaaliwa ikishinda moja kwa moja itatangazwa Bingwa wa Kombe hilo kwa Msimu wa Pili Mfululizo.