Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia maisha wanafamilia wawili kujishughulisha na mpira wa miguu.
Mwenyekiti waKitayosce FC, Yusuph LKitumbo na Kocha wa moira wa miguu Ulimboka Mwakingwe wametiwa hatiani kwa kosa la upangaji matokeo.
Wawili hao walijihusisha na kitendo cha upangaji wa matokeo katika mechi ya Ligi ya Championship kati ya Fountain Gate FC na Kitayosce FC iliyochezwa Aprili 29 Mwaka huu.
Kamati ya Maadili Katika kikao chake kilichofanyika mei 11 mwaka huu imewatia hatiani kwa kuzingatia ibara ya 73(9)(b) ya kanuni ya Maadili ya TFF, Toleo la 2021
Kitumbo alikahidi kufika mbele ya kamati bila kutoa udhuru wowote wa maandishi ya kupokea wito, wakati Mwakigwe aliwasilisha utetezi wake kwa njia ya nmaandishi.
Uamuzi kamili utatolewa kwa maandishi kwa pande husika katika mashauri hayo mawili.