Meneja Habari wa Simba SC amefunguka kuwatoa hofu wadau na mashabiki wa klabu hio kuhusu kuondoka kwa wachezaji nyota ambao wamekuwa wakitajwa kuhusishwa zaidi na usajili katika vilabu vingine.
Ameeleza kuwa wachezaji wote watakao hitajika na klabu hio watasalia hata kama mikataba yao itakuwa imekamilika taratibu mpya itafuata kuwabakisha.
“Unapokua na wachezaji wenye Quality kubwa tegemea tetesi nyingi kipindi cha usajili Mohammed Hussein anatakiwa na timu za South Afrika, Manula anukia Azam Fc, Baleke anatakiwa na timu za Ulaya Niwathibitishie Wana Simba hakuna mchezaji ambae yupo kwenye mipango yetu ataondoka, Wale waliomaliza mkataba na tunawahitaji watasalia Maboresho tunayoyafanya ni pamoja na kuwabakisha wale tunaowahitaji”