WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameita Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya ongezeka la utapeli wa mtandaoni. Akizungumza jijini Dodoma leo, Mei 19, 2023 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/24, Nape amesema tatizo la utapeli kwenye mitandao ya simu za mkononi bado ni kubwa nchini.
Pia ameitaka TCRA kutafuta namna ya kuzuia jumbe fupi zinazotumwa bila idhini au matakwa ya mteja. Nape aliwasilisha maoni na ushari wa wadau kuhusu uboreshwaji wa taasisi ambapo miongoni mwa maoni hayo ni kuitaka wizara ishirikiane na makampuni ya mitandao ya simu pamoja na Jeshi la Polisi ili kumaliza tatizo la utapeli wa kimtandao ikiwamo kufungia namba za matapeli.