Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino huku viongozi mbalimbali wakishuhudia katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuingia Ofisini kwake Chamwino Mkoani Dodoma baada ya uzinduzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwenye Jukwaa wakati Wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino.