Kundi la Sauti Sol kutokea nchini Kenya limetangaza kuwa litasitisha kufanya kazi pamoja kama kundi kwa muda usiojulikana baada ya kufanya kazi pamoja kwa miaka mingi.
Kundi hilo lililoundwa na jumla ya wasanii wanne wameweza achia nyimbo nyingi zinazopendwa na mashabiki kutoka maeneo tofauti duniani pindi wakiwa pamoja ambapo baadhi ya nyimbo zao ziliweza kufanya vizuri zaidi kwa kuwa na idadi ya wasikilizaji wengi zaidi kupitia majukwa ya muziki mdalimbali ya mitandaoni.
Sauti Sol kabla ya kusitisha muunganiko wao watafanya ziara ya dunia kutumbuiza katika mataifa mbalimbali kwa mara ya Mwisho. #KoncepttvUpdates