Wydad Casablanca AC ya Sven Vandenbroeck yafanikiwa kutinga Fainali katika Michuano ya Kalbu Bingwa Afrika CAFCL baada ya kuibuka na ushindi wa faida ya magoli ya ugenini 2-2 dhidi ya wenyeji wao wa mchezo Mamelodi Sundown kutokea Afrika Kusini katika katika mechi ya Marudiano Nusu Fainali iliyocheza hii leo Mei 20, 2023.
Ushindi huo mnono wa magoli kwa Wyadad imewafanya washiriki fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wakutane mara nyingine dhidi ya Al Ahly ambayo hapo jana ilifanikiwa kuwaondosha Esparence De Tunis kwa jumla ya goli 4-0.