
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma hapo jana amesema baada ya kukamilika kwa Ikulu sasa wanatarajia kujenga jengo la kisasa “Samia Complex” ndani ya eneo hilo kubwa la Ikulu lenye ekari 8473 na tayari michoro ipo tayari ambapo kwa sasa wanashughulikia kutafuta fedha ili ujenzi uanze.
Rais Dkt. Samia amesema “Eneo hili bado kuna kazi ya kufanya na hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la kisasa ambalo Wasaidizi wangu wameliita Samia Complex ambalo litakuwa na ukumbi wa mikutano wa Watu Elfu mbili mpaka Elfu tatu, nyumba za Viongozi hasa Majirani zetu wa EAC na SADC kutakuwa na Zanzibar Lounge, East Africa Lounge, uwanja wa golf, viwanja vya michezo, njia za ndege na sehemu za historia za Viongozi wa Nchi zetu”