Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi mpya wa Mabalozi 8 katika kuiwakilisha Serikali juu ya Utekelezaji wa majukumu yake.
Amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamndi ya Jeshi la Wazamiaji (JWTZ).
Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya Uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
Amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudi Arabia.
Amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
Amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo,Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania Uturuki.
Amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Mwndamizi wa Waziri Mkuu Hotuba.
Amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.