Mwamuzi Szymon Marciniak ambaye aliwahi chezesha Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Ufaransa amechaguliwa kuwa ndiye atakeamua mchezo wa Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA baina ya Manchester City na Inter Milan.
Szymon Marciniak ni mwamuzi wa kulipwa wa mpira wa miguu kutoka Poland. Anachukuliwa kuwa mmoja wa waamuzi wa kimataifa waliokadiriwa kuwa vizuri sana katika kizazi chake.