Menejimenji ya Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kimekanusha Vikali juu uvumi wa taarifa zilizoenea mitandaoni zikikusisha chuo hicho kutoa elimu kupitia Programu za kitaaluma zilizopitwa na wakati.
Menejimenti imeueleza umma kuwa imegundua kuna taarifa zilizosambaa mtandaoni zikieleza kuwa vyuo vingi nchini Uganda vinatoa Programu za kitaaluma zilizopitwa na wakati ikiwemo chuo hicho.
Menejimenti ya Chuo hicho imekanusha kwa kusema kuwa chuo chao hakina Programu za kitaaluma zilizopitwa na wakati kwani kila wakati kuna mabadiliko ambayo hufanywa kupitia idara za chuoni pamaoja na Kamati maalum zinazounganisha vyuo mbalimbali nchini humo.
Aidha imegundua kipengele cha Programu za kitaaluma 89 zilizoaminika kupitwa na wakati na zilizoorodheshwa katika taarifa zinazoendelea mtandaoni kuwa hazitolewi kabisa kwa sasa katika chuo chao.
Chuo hicho kimesema kinawahakikishia wadau pamoja na wanachuo kuwa Programu zote za kitaaluma 331 zinazotolewa katika hata tawi la chuo cahake cha Biashara (MUBS) zimepitishwa na kuthibitishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Juu la Nchini humo.