Gavana wa jimbo la Florida nchini Marekani Ron Desantis aanza kampeni zake za kugombania Urais wa nchi hiyo katika uchaguzi Mkuu wa 2024 kwa kupitia mtandao wa Twitter.
Desantis amepewa nafasi ya kufanya hivyo na mmiliki wa mtandao huo, Elon Musk ambaye naye atakuwepo katika tukio hilo leo Jumatano.
Desantis , mwenye miaka 44 ni mpinzani wa Rais wa zamani Donald Trump katika kinyang’anyilo cha kuwania nafasi hiyo kupitia chama cha The Republican.
Kujitokeza kwake Gavana huyo kutazima uvumi kuhusu gavana huyo kuwa na nia ya kugombea au la.
Tayari Trump ameonesha kuwa anayo nia ya kugombania tena nafasi hiyo licha ya kuandamwa na kashfa za ubakaji ambazo amedai zipo kisiasa kwa nia ya kumchafua.
Aidha, Trump mpakahadi wakati huu anaongoza kwa kura za maoni katika chama chake juu ya mchakato wa kumtafuta nani atapambana na Rais wa sasa Joe Biden kutoka chama cha Democrat katika uchaguzi huo utakaofanyika mwezi Novemba mwakani.