
Afisa Habari wa Young Africans SC Ally Kamwe, Mkurugenzi wa Wanachama na mashabiki Haji Mfikirwa pamoja na maofisa wa Yanga wametembelea chuo cha IFM kilichopo Jijini Dar es Salaam na kukutana na wanafunzi ambao ni mashabiki wa Yanga wanaosoma chuoni hapo.
Aidha msafara huu umetoa zawadi ya tiketi kwa wanafunzi watakaohudhuria Benjamin Mkapa kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho #CAFCC dhidi ya USM Alger utakaopigwa jumapili hii
