Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema limefanikiwa kumkamata Mtuhumiwa aitwaye Isack Robertson (45) Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Mke wake aitwaye Jackline Mkonyi (38) Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha.
Mtuhumiwa huyo amekamatwa jana katika maeneo ya Himo Mkoani Kilimanjaro, anaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
RPC wa Arusha, Justine Masejo amesema “Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa onyo kwa baadhi ya Watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika Familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani kwa kuendelea kufanya vitendo hivyo, hatutasita kuwakamata”
“Pia niwaombe Wananchi popote walipo wasifumbie macho vitendo viovu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu katika maeneo yao ili kukomesha matukio hayo”