Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya awali kuhusu majeruhi Mkapa Stadium Dar es salaam ambapo amesema hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea majeruhi 30 ambapo Mwanaume mmoja mwenye umri wa takribani miaka 40 amefariki.
Tukio hilo limetokea leo hii ikiwa ni Siku ya Mchezo wa kwanza wa Fainali ya CAFCC baina ya Yanga na USM Alger uliochezwa katika Uwanja wa Mkapa wakati Wadau na mashabiki wa timu hio walipokuwa wamesongamana katika kuwania kupata nafasi ya kuingia ndani ya uwanja kushuhudia mtanange huo.
“Taarifa ya Awali: Kuhusu Majeruhi Mkapa Stadium DSM. Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea Majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40.
Majeruhi wengine wanaendelea vizuri wana majereha madogomadogo, wanaendelea na vipimo. Aidha timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa DSM ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine. Timu ya Wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo standby kupokea na Kuwahudumia majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi.” Ummy Mwalimu – Waziri wa Afya
#KoncepttvUpdates