Mshambuliaji wa nchini Misri anayekipiga mnamo Klabu ya Liverpool, EPL Mohamed Salah,30 amedhihirisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa klabu yao kukosa kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao 2023/24.
Ushindi wa Man United wa goli 4-1 dhidi ya Chelsea Alhamisi (Mei 25) uliashiria Liverpool haiwezi kumaliza katika nne bora na rasmi hawatacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kikosi hicho chini ya Jurgen Klopp hakijafanya vizuri msimu mzima na sasa kitashiriki kwenye Ligi ya Europa.
Nyota huyo amekiri timu hiyo imeshindwa na imewaangusha mashabiki msimu huu kwa kutomaliza katika nafasi nne za juu.
Na hilo limemfanya Salah kutopendezwa nalo na amesema: “Nimevunjika moyo kabisa. Hakuna kujitetea katika hili.
“Tulikuwa na kila kitu tulichohitaji ili kufikia Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.”
Katika msimu wa kusikitisha, Salah bado amefunga mabao 30 na amebakiza moja pekee kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kufunga mabao 20 na asisti 10 ndani ya misimu mitatu, ambayo ingevuka rekodi aliyowekwa na Thierry Henry