
Akipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Afya unaoendelea jijini Geneva Uswisi, Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuthamini mchango wa nchi ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria kupitia kadi ya alama, huku akisisitiza kuendelea kushirikiana na wadau wengine ili kuutokemeza ugonjwa huo.
Akiwa katika Mkutano huo, Mhe. Nassor Mazrui ametumia nafasi hiyo kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Viongozi wa Afrika wa kupambana na ugonjwa wa Malaria na Magonjwa yasiyopewa kipaumbele (African Leaders Malaria Alliance- ALMA).
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akiambatana na Wataalamu wengine wametumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa chama cha wataalam wa dawa za usingizi (Anaesthesia) duniani, katika kikao cha pembezoni mwa mkutano mkuu huo ili kuona namna gani wanaweza shirikiana na nchi ya Tanzania kuboresha huduma za macho.
Katika mazungumzo hayo, wamekubaliana kwa pamoja kushirikiana kutafuta raslimali za kuwezesha kuimarisha huduma za usingizi nchini ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa watoa huduma ili kutoa huduma bora kwa ufanisi wa juu.