Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anatarajia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ukikamilika mwishoni mwa msimu wa 2023-24. (Viaplay, viaManchester Evening News)
Nyota huyo kwa aina ya uchezaji wake unampa nafasi kubwa ya kuonekana bado ana umuhimu mkubwa wa kusalia katika klabu hio ingawa katika suala la upatikanaji wa matokeo mazuri kwa mechi mfululizo umekuwa ni bado wa kusuasua sio kama ilivyokuwa hapo awali ikiaminika kwa asilimia za juu na wadau pamoja na mashabiki zake.
Rashford amefanikisha kuipatia klabu yake jumla ya magoli 30 katika msimu huu wa Ligi kuu EPL na ndio maana siku chache kupitia ukurasa wa mtanadao wa kijamii wa Twitter hakusita kuishukuru klabu yake na wachezaji kwa kufanikisha iwe hivyo.
— Marcus Rashford (@MarcusRashford) May 25, 2023