Klabu ya Yanga leo hii imekubali Kichapo cha goli 1-2 kutoka USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa kwanza Michuano ya Fainali Kombe la Shirikisho CAFCC ikiwa katika Ardhi ya Nyumbani.
Licha ya jitihada zilizoonyeshwa na klabu hio katika kuwania kuifunga timu pinzani ndani ya Dakika 90 hali imekuwa sio shwari kwa upande wao kwa kuwa wameruhusu kupoteza nafasi muhimu wakiwa ndio wenyeji wa mchezo.
Hapo sasa inatazamiwa zaidi klabu hio kujiandaa vyema ili kuweza kuifunga USM Alger Goli 3 au ikiwezekana zaidi ya hapo endapo, wapinzani wao hawatawapa nafasi ya kutikisa nyavu zao kwa kuongeza magoli zaidi.
USM Alger inarudi kwao kifua mbele kwa jumla ya faida ya Goli 1 la ugenini, wakisubiria mchezo wa marudiano mambo yatakuaje dhidi ya Yanga.