Golikipa nambari moja Simba SC na Taifa la Tanzania Aishi Manula aripotiwa kuwa yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya kupatiwa matibabu ya Nyama za Paja kwa siku za hivi karibuni.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC amefunguka kuhusu taarifa hio kuhusu Nyota huyo kuwa yupo chini humo kwajili ya kupatiwa matibabu ameandika “Kipa wa Taifa Aish Salum Manula yupo Nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya nyama za paja Mungu amjaaalie nyanda wetu matibabu yake yaende vizurii”
Manula amekosekana uwanjani tangu mechi ya kwanza ya kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya Michuano Nusu Fainali Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Wydad Casablanca dhidi ya timu yake, hadi sasa ni muda mrefu umepita.
Hapo nafasi ya kulinda lango la timu ya Simba alichuliwa na Golikipa nambari 3 wa klbu hio Ally Salim ambaye alikuwa sio mzoefu kabisa katika kudakia Michuano ya namna hio CAF lakini alionesha uwezo kulingana na timu yake ilivyoweza kumuamini.
Licha ya matumaini ya Wadau na mashabiki wengi wa klabu hio kuzania kuwa hali ya mchezaji huyo itaimalika haraka na kurejea mchezoni bado hali inaonyesha kuwa Manula hayuko sawa na ndio maana ameenda chini huko kupatiwa matibabu na uangalizi wa karibu kutoka kwa madaktari bingwa.