Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo, amepiga marufuku Mkoa wa Iringa kuwa sehemu ya kupata mabinti wa kazi na badala yake Mkoa huo upate sifa kwa kutoa mabinti wenye taaluma mbalimbali nchini.
“Iringa sio mkoa wa kupata mabinti wa kazi badala yake watafute madaktari, wauguzi ,mainjinia na mabinti wenye taaluma mbalimbali, hivyo nawaomba wananchi kuhakikisha mabinti na vijana wote wanaenda shule” amesema Chongolo. #KoncepttvUpdates