Meneja mpya Chelsea Mauricio Pochettino tayari amemwambia Todd Boehly kuwa hataki mchezaji mwenye umri wa miaka 23 kwenye kikosi chake cha Chelsea msimu ujao.(90 Min)
Joao Felix ahusishwa zaidi katika mpango huo wa kutowepo katika kikosi hicho cha Chelsea msimu ujao. João Félix hatabaki Chelsea msimu ujao. Pochettino ameamua, João anarejee timu yake ya Atléti. “Tumearifiwa kwamba Poch hamhesabii João Félix kusalia Chelsea. Atarudi hapa, tutaona… hatujapanga chochote”, rais wa Atlético Cerezo ametangaza. (Fabrizio Romano)
Felix alijiunga na Chelsea mwezi Januari kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita ghali ambao haukuwa na chaguo la kununua, lakini viongozi wa klabu walikuwa kwenye mazungumzo na Atletico kuamua gharama ya uhamisho wa kudumu.
Mazungumzo hayo yalianza wakati Graham Potter akiwa madarakani, hata hivyo, na huku Mauricio Pochettino sasa akiwa dimbani, hali imebadilika na ni Muargentina huyo aliyetoa wito wa mwisho kuhusu mustakabali wa Felix.
“Ukweli ni kwamba siwezi kukuambia mpango huo na Joao,” Cerezo alisema. “Ni habari tuliyokuwa nayo jana, kwamba kocha mpya hamtegemei Chelsea.
“Bado hatujapanga lolote, Joao ni mchezaji wa Atletico sasa.”